Mtoto aliyepotea apatikana amefariki ndani ya gari la kasisi wa Mombasa

0
1080

Mombasa,KENYA: Polisi likoni wameanzisha uchunguzi kufuatia tukio ambalo mtoto wa miaka sita amepatikana amefariki ndani ya gari la kasisi.

Polisi wanasema mtoto huyo alikuwa na wengine kanisani siku ya jumapilli lakini akaripotiwa kuwa amepotea.

Baadae Wazazi wake walimtafuta na walipomkosa wakaenda kuripoti katika kituo cha polisi cha likoni.

Mapema leo zoezi la kumtafuta lilianzishwa na waliporejea kanisani humo wakampata amefariki ndani ya gari la kasisi wa kanisa hilo.

Mkuu wa upelelezi likoni henry Ndombi anasema wameanzisha uchunguzi.

Comments

comments