Mwili wa mwanafunzi aliyezama baharini wapatikana Kilifi

0
1126

Kilifi,KENYA: Mwili wa mvulana wa umri wa miaka 14 aliyezama baharini Jumamosi huko Magarini hatimaye umepatikana.

Afisa mkuu wa polisi eneo hilo Gerald Barasa amesema mvulana huyo kwa jina Chui Josphat alizama eneo la Che Shale huko Magarini alipokuwa akiogelea na wenzake.

Mwili wa mvulana huyo unahifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali kuu ya Malindi.

Kwingineko idara ya usalama huko Magarini kaunti ya Kilifi imeonya kuwachukulia hatua kali za kisheria wote wanaohusika na mauaji ya wazee kwa tuhuma za uchawi.

Kulingana na afisa mkuu wa polisi eneo la Magarini Gerald Barasa, ni jambo la kuhuzunisha kuona wazee wasiokuwa na hatia wanauawa kwa kisingizio kuwa ni wachawi.

Barasa ameitaka jamii katika eneo hilo kuibuka  na mbinu mbadala ya kusuluhisha matatizo yao badala ya kuwauwa wazee.

Comments

comments