Wanafunzi wa vyuo vikuu hapa Mombasa wataandamana iwapo aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi Sonko ataendelea kuzuiliwa.
Wanafunzi hao wamekosoa serkali kwa madai ya kuwakamata na kuwashtaki baadhi ya viongozi wanaopinga BBI.
Aidha wamemtaka naibu rais William Ruto kuwatetea viongozi wanaomuunga mkono ambao wamekuwa wakihangaishwa na serikali.