Mzee wa miaka 60 auawa na Kiboko Magarini

0
1484

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 ameuawa baada ya kuvamiwa na kiboko katika eneo la Bate huko Magarini kaunti ya Kilifi.

Mzee huyo kwa jina Charo Kilulu Kombo anadaiwa kuvamiwa na kiboko wakati akiitoka nje ya nyumba kuangalia ngombe wake ambapo alivamiwa na kiboko anayeaminika kutoka mto Sabaki takriban umbali wa kilomita moja kutoka kwa boma lake.

Akithibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa polisi huko Magarini Gerald Barasa amesema mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali kuu ya Malindi.

Comments

comments