Niarobi,KENYA: Chama cha jubilee kimewateua watu 15 akiwemo katibu mkuu wa zamani kuwa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki EALA.
Wao ni pamoja na aliyekuwa karani wa bunge Justin Bundi na aliyekuwa katibu wa wizara ya usalama wa ndani Mutea Iringo.
Aidha mbunge wa zamani Simon Mbugua aliyemwachia mbunge wa sasa Yusuf Hassan tiketi ya jubilee pia ameteuliwa kwa bunge hilo.
Wengine ni Eunice Wanjiru Karanja, Irene Cherop Masit, Nelson Dzuya miongoni mwa wengine.
Hii hapa orodha ya majina ya walioteuliwa;
- Joe Muriithi Muriuki
- Mutea Iringo
- Eunice Wanjiru Karanja
- Abubakar Ogle
- Adan Mohamed Nooru
- Simon Mbugua
- Irene Cherop Masit
- Justin Nthiiri Bundi
- Nelson Dzuya
- Naomi Jillo Waq
- Chepkemoi Saida Stacey
- Florence Sergon
- Justus Mate
- Pius Atok Ewoton