Walimu kupata nyongeza ya mishahara

0
1618

Nairobi,KENYA: Walimu wataanza kupokea nyongeza yao ya mshahara mwezi wa saba mwaka huu.

Tume ya huduma kwa walimu TSC inasema serikali imetoa shilingi bilioni 13.8 kutekeleza mpango huo wa nyongeza ya mishahara.

Aidha nyongeza hiyo itakua ikitolewa kwa awamu.

Mwaka jana walimu waligoma kwa miezi kadhaa kutaka nyongeza ya mishahara kama walivyoelewana na serikali.

Kenya ina takriban walimu 305,000 wa umma.

Hayo yakijiri maafisa wa polisi pia wanatarajiwa kupokea nyongeza ya mishahara mwezi huo wa saba.

Comments

comments