Nairobi,KENYA:Kenya imeitisha Uchina mkopo mwingine wa shilingi bilioni 370 ili kukamilisha ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Naivasha hadi Kisumu.
Rais Uhuru Kenyatta anaongoza ujumbe wa Kenya nchini Uchina kupata mkopo huo kutoka benki ya Exim .
Reli hiyo itakuwa ya kilomita 270 kutoka Naivasha hadi Kisumu.
Rais Uhuru Kenyatta pia anatarajiwa safari ya kwanza ya gari moshi za SGR kutoka Nairobi hadi Mombasa mwezi ujao.
Mradi wa kwanza wa Mombasa hadi Nairobi uligharimu shilingi bilioni 327