Waandishi wa Baraka FM wazoa tuzo za wanahabari

0
1448

Nairobi,KENYA:Baraka FM kwa mara nyingine imejizolea sifa tele katika tuzo za waandhishi wa habari zilizoandaliwa siku ya jumatano mjini Nairobi na baraza la vyombo vya habari.

Maripota Diana Wanonyi na Joseph Jira walishinda tuzo katika hafla ya kusherehekea uhuru wa vyombo vya habari.

Diana aliibuka mshindi mara mbili kwa kuandika makala kuhusu uhuru wa vyombo vya habari hapa pwani na katika kitengo cha biashara.

Naye Jira alishinda tuzo katika kitengo cha uongozi na utawala.

Makala yake iliangazia juhudi za wanawake kukabili itikadi kali katika jamii.

Jira pia aliibuka wa pili katika kitengo cha biashara.

Francis Ontomwa na Francis Mutalaki wote wa KTN, ni miongoni mwa wanahabari wa pwani walioshinda tuzo.

Kila mwaka, stesheni ya Baraka FM  hujizolea sifa tele katika mashindano ya uandishi kupitia wanahabari wake ambao wamebobea.

Washindi hutuzwa hundi na vyeti.

Comments

comments