Bei ya unga na mkate kushuka kufuatia bajeti kusomwa

0
1826

Nairobi,KENYA:Bei ya unga wa mahindi na mkate inatarajiwa kushuka.

Hii ni baada ya serikalu kuondoa ushuru kwa bidhaa za unga na mkate katika bajeti iliyosomwa na waziri wa fedha Henry Rotich.

Hata hivyo Rotich ameonya kampuni za unga iwapoa hazitapunguza bei akisema serikali itazichukulia hatua.

Bei ya sasa ya unga wa sima ni shilingi 150 kwa kilo mbili.

Mkate mzima unauzwa kati ya shilingi 55-60.

Comments

comments