Raila asema Kalonzo haondoki NASA liwe liwalo!

0
1053

Nairobi,KENYA:Kinara wa Nasa Raila Odinga amesema muungano huo uko imara huku akipuuza tetesi kuwa utasambaratika.

Raila anasema kuwa vinara wote wa NASA wako dhabiti huku akipuuzilia mbali habari kuwa kinara mwenza Kalonzo Musyoka atahama muungano huo.

Kulinagana na Raila, Kalonzo amemhakikishia kwa njia ya simu kuwa bado ana imani na NASA.

Aidha amekashifu serikali kuhusu namna inavyo mkabili gavana Joho kuhusu stakabadhai zake za masomo.

Kinara huyo wa ODM anadai kuwa serikali inampiga vita Joho kwasababu ya mazoeya ya kusema ukweli.

Comments

comments