Sonko adai jubilee ina njama ya kumnyima tiketi

0
1337

Nairobi,KENYA:Seneta wa Nairobi Mike Sonko anadai kuwa kuna njama ya kumnyima nafasi ya kugombea ugavana wa Nairobi kwa tiketi ya chama cha jubilee.

Sonko anadai kuwa hio inatokana na kuwa amenyimwa cheti cha maadili kutoka kwa polisi na pia jubilee inamwitisha cheti chake rasmi cha kidato cha nne KCSE akihisi kuwa ni mpango wa wapinzani wake ndani ya jubilee ili asishiriki kura ya mchujo.

Anadai kuwa alituma ombi la kupata stakabadhi hiyo kupitia mtandao lakini kufikia sasa hajapata.

Kulingana na Sonko, kauli ya kumnyima stakabadhi hiyo ya maadili mema, imetoka kwa afisa wa ngazi ya juu katika ofisi ya rais.

Wakati huo huo mbunge maalum wa Nairobi Johnston Sakaja sasa ametangaza kujiondoa kutoka kinyang’anyiro cha ugavana wa Nairobi.

Badala yake anasema atagombea kiti cha useneta.

Alisema hayo alipowasilisha makaratasi yake ya uteuzi kwa makao makuu ya jubilee mjini Nairobi akiandamana na mwakilishi wa wanawake Rachel Shebesh, na mbunge wa Gatundu kusini-Moses Kuria.

Mbunge wa Dagoretti kusini Dennis Waweru, aliyekuwa mbunge wa Starehe  Margaret Wanjiru pamoja, seneta Gidion Mbuvi na Peter Kenneth wote wanapania kugombea kiti hicho cha ugavana wa Nairobi kupitia chama cha jubilee.

 

 

 

 

 

Comments

comments