Malindi,KENYA: Washukiwa 6 wa ugaidi wamekamatwa na polisi mjini Malindi.
Sita hao ambao ni watu wa familia moja, walikamatwa ijumaa usiku mjini Malindi.
Duru za habari zinasema kuwa walikamtwa ndani ya nyumba yao katika oparesheni ya polisi wa kupambana na ugaidi ATPU.
Maafisa hao walivunja madirisha ili kuingia kwa nyumba hiyo iliyokuwa na washukiwa hao ambapo walitiwa nguvuni.
OCPD wa Malindi – Matawa Muchangi alidhibitisha tukio hilo akisema taarifa kamili zitatolewa baada ya washukiwa kuhojiwa zaidi.