Hakuna maandamano yanayoruhisiwa wakati huu taifa linapambana na janga la corona.
Huo ni usemi wake Inspector-Generali wa polisi Hillary Mutyambai ambaye ameonya wananchi dhidi ya mikusanyiko.
Akijibu masuali ya wakenya katika twitter, Mutyambai amesema kila mkenya sharti atii maagizo ya wizara ya afya ya kujikinga na corona.
Hii inafuatia kutiwa mbaroni kwa wanaharakati kadhaa walioandamana kushtumu kashfa ya ufujaji wa fedha za kupambana na janga la corona.