Wanawake 7 wafariki baada ya kugongwa na lori Bungoma

0
1257

Watu 7 wengi wao wanawake wamefariki baada ya kugongwa na lori katika soko la Kaburengu kwenye barabara ya Webuye-Eldoret.

Hii ni baada ya lori hilo kuwagonga wanawake hao ambao ni wachuuzi wa kando ya barabara.

Hayo yakijiri ajali zingine mbili zimetokea kwenye barabara ya Mombasa-Kilifi karibu na Mombasa cement.

Ajali ya kwanza imehusisha lori na gari la kibibnafsi huku madereva wa magari hayo wakijeruhiwa.Magari hayo yamegongana ana kwa ana.

Katika kisa cha pili ambacho kimetokea mita 200 kutoka eneo la ajali ya kwanza, watu wawili pia wamejeruhiwa baada ya magari ya kibinafsi kugongana.

Comments

comments