COVID-19: Hofu yatanda bandari ya Mombasa

0
1273

Mombasa sasa imeripoti visa 18 vya coronavirus tangu mlipuko wa ugonjwa huo uripotiwe nchini.

Aidha kifo cha mtu mmoja pia kilitokea hapa Mombasa.

Ursula Buluma mwenye miaka 58 alikuwa mfanyakazi wa KPA na alifariki kutokana na ugonjwa huo katika Mombasa Hospital.

Baadae alizikwa katika makaburi ya Mbaraki hapa Mombasa.

Hayo yakijiri, hofu imetanda katika bandari ya Mombasa kutokana na hofu ya coronavirus, baada ya mfanyakazi mwingine kuripotiwa kuambukiwa ugonjwa huo.

Wiki jana, mfanyakazi wa KPA alifariki na kuzikwa baada ya kuugua ugonjwa huo wa coronavirus.

Hofu hiyo imetokana na kuwa wafanayakazi hao walitangamana na wenzao bandarini humo kwa muda.

Lakini afisa wa mawasiliano katika  KPA – Haji Masemo ameambia Baraka fm kwamba huenda hali sio mbaya kama inavyodhaniwa .

Comments

comments