Wakazi wa Taita Taveta wataka KWS kuwapa mapato ya mbuga

0
1715
KWS Rangers

Viongozi wa kaunti ya Taita Taveta wameanzisha mchakato wa kukusanya sahihi kwa lengo la kuwasilisha waraka kutaka kugawana mapato ya mbuga za wanyama za Tsavo na KWS.

Akizungumza katika wadi ya  Mboghoni kaunti ndoogo ya Taveta, gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja amesema KWS inafaa kuwalipa wenyeji kutokana na uharibifu wa mimea na makazi ambao hutekelezwa na wanyamapori.

Amewataka wawakilishi wadi kuhakikisha wanakusanya sahihi hizo kutoka wadi zao ili kufanikisha mchakato huo.

Wakati huo huo MCA wa Sagala Godwin Kilele ameunga mkono mchakato huo akisema raia wameumia kwa muda mrefu.

Comments

comments