Gavana Obado apewa dhamana katika kesi ya mauaji

0
1187

Gavana wa Migori Okoth Obado ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni tano pesa taslim.

 Jaji anayesikiliza kesi hiyo bi. Jessie Lesiit, pia ameonya Obado  dhidi ya kutishia familia ya marehemu Sharon Otieno ama kusafiri umbali wa kilomita 20 kutoka Migori.

Pia ameagizwa kukabidhi pasipoti yake ya usafiri kwa mahakama.

Obado anakabiliwa na  kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo-Sharon Otieno.

Kwingine mwanahabari Jacque Maribe na mpenzi wake Joseph ‘Jowie’ Irungu wanatarajiwa kortini leo kusikiliza ombi la kutaka kuachiliwa kwa dhamana.

Maribe na Irungu wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya Monica Kimani ambaye alikuwa mfanyabiashara.

Wawili hao walikana mashtaka ya mauaji na wamekua wakizuliwa katika gereza la Lang’ata na Industrial area.

Comments

comments