Jacque Maribe na Jowie kushtakiwa kwa mauaji

0
1316

Nairobi,KENYA: Mwanahabari  Jacque Maribe na mchumba wake Joseph Irungu wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu mashtaka ya mauaji.

Hii ni baada ya Maribe kufanyiwa uchunguzi wa akili ambapo imebainika kuwa yuko sawa kujibu mashtaka hayo.

Mwanahabari huyo amekuwa akizuiliwa katika gereza la wanawake la Lang’ata huku Irungu akizuiliwa gereza la Industrial area.

Wawili hao wanashtumiwa kumwua mwanamke kwa jina Monica Kimani jijini Nairobi, aliyepatikana amekatwa shingo mwezi septemba.

Comments

comments