Hakimu wa Mombasa amnunulia mshukiwa ‘chakula’

0
1540

Mombasa,KENYA: Katika kisa kisichokuwa cha kawaida, hakimu mkuu wa mahakama ya Mombasa amemnunulia mshukiwa aliyefikishwa mbele yake chakula cha mchana.

Hakimu Henry Nyakweba ameshangaza mahakama baada ya kumpa mshukiwa bi Bi. Everlyn Obera noti ya shilingi 100 ya kununua chakula baada ya mshukiwa kushindwa kupaza sauti wakati akihojiwa kutokana na njaa ya siku tano.

Hakimu Nyakwemba pia aliwaomba watu waliokuwa wakihudhuria kesi kortini kuchangisha pesa ambapo shilingi 1,100 zilichangwa kwa muda mfupi kisha mwanmke huyo akapewa.

Bi. Obera alidaiwa kumlaghai Haluloa Charo shilingi elfu 9 eneo la Miritini SGR akidai akaunti yake ya benki imefungwa hivyo anatafuta pesa kuifungua tena.

Aidha Nyakweba ameamuru mshukiwa aachiliwe huku akishtumu polisi kwa kukosa utu kwa kumnyima mshukiwa chakula kwa siku tano.

 

Taarifa yake Emmanuel Mchonji

Comments

comments