Raila atanyongwa akijiapisha kama rais,Muigai aonya

0
1577

Nairobi,KENYA: Kinara wa NASA Raila Odinga anajiweka katika hatari ya kunyongwa iwapo ataendelea na tishio lake la kuapishwa kama rais wiki ijayo.

Hayo ni kwa mujibu wa mwanasheria mkuu Githu Muigai.

Muigai anasema hakuna mtu mwengine atakayeapishwa kama rais baada ya rais Uhuru Kenyatta kuapishwa.

Amedokeza kuwa iwapo Raila ataapishwa tarehe 12 wiki ijayo, atakuwa ametenda kosa la uhaini na adhabu ya uhaini ni kifo.

Pia amekosoa mpango wa Nasa kubuni mabunge ya wananchi akidai ni mpango wa kutumia vibaya pesa za serikali za kaunti.

Muungao wa Nasa tayari unaendelea na mikakati ya kumuapisha Raila Tarehe 12.

Comments

comments