Mahakama ya juu yaidhinisha ushindi wa rais Kenyatta

0
1838
Rais Uhuru Kenyatta.

Nairobi,KENYA: Mahakama ya juu zaidi leo imeidhinisha ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kufuatia marudio ya uchaguzi wa oktoba tarehe 26 ambayo wafuasi wa Nasa walisusia.

Majaji wa mahakama hiyo wakiongozwa na jaji mkuu David Maraga wamesema kesi hizo hazikuwa na uzito.

Rais Uhuru Kenyatta sasa ataapishwa rasmi tarehe 28 wiki ijayo kuhudumu muhula wake wa pili.

Hafla hiyo inatarjiwa kufanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani jijini Nairobi.

Mahakama ya juu zaidi imeidhinisha ushindi wake katika marudio ya kura ya urais kwa kutupilia mbali kesi tatu zilizowasilishwa dhidi yake.

Wakati huo huo wafuasi wa chama cha Jubilee huko Malindi kaunti ya kilifi wamesherehekea ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta kufuatia uamuzi wa mahakama ya juu nchini ya kutupilia mbali kesi zilizowasilishwa kupinga matokeo ya urais ya Oktoba 26.

Wakiongozwa na aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge wa Malindi kwa tiketi ya Jubilee Philip Charo amesema ushindi wa Raisi Kenyatta ni ushindi wa kenya nzima haswa kwa wafuasi wa chama cha Jubilee huku akiwataka Wakenya wote kuunga mkono viongozi wa serikali kuu kwa maendeleo zaidi.

Hata hivyo amekashifu viongozi wanaoendeleza mchakato wa eneo la pwani kujitenga akiitaja kama ndoto.

Wakati huo huo baadhi ya wafuasi wa Nasa huko Malindi wameeleza kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama hiyo wakiutaja kama wa upendeleo.

KWALE

Na huko Kwale Hisia tofauti zimeibuka baina ya viongozi wa jubilee na wale wa mrengo wa nasa kuhusisna na maamuzi ya mahakama kuhusu kesi ya ushindi wa raisi Kenyatta.

Viongozi wa Nasa wakiongozwa na mwakilishi wa wanawake kaunti yak wale Zuleikha Hassan wanasema maamuzi hayo hayatabadilisha msimamo wa mrengo wa  nasa kivyovyote vile.

Lakini wale wa jubilee wakiongozwa na aliyekuwa mwakilishi wa wanawake Zainab Chidzuga wamesherehekea  wakisema ushindi wa Kenyatta ni ujio wa amani kenya.

Kadzo Michael na Lawrence Sita wamechangia taarifa hii

Comments

comments