Mwanafunzi aanguka ndani ya shimo la choo na kufariki huko Jomvu

0
1371

Mombasa,KENYA: Mwanafunzi wa chekechea ameaga dunia baada ya kuanguka ndani ya shimo la choo katika shule ya msingi ya Jomvu hapa Mombasa.

Walioshuhudia wanasema mwanafunzi huyo mvulana alikuwa akicheza na wenzake na alipoenda kujisaidia akaanguka ndani ya shimo hilo na kufariki.

Wakaazi wamesababisha vurugu shuleni humo na kuvunja ofisi ya mwalimu mkuu na madarasa kadhaa  kwa hasira.

Mkuu wa polisi Changamwe Peter Omwana amesema uchunguzi umeanzishwa na watakaopatikana kukiuka sheria watachukuliwa hatua kali.

Amewataka wazazi na wakaazi kuwa watulivu huku polisi wakishughulikia suala hilo

Comments

comments