Wafuasi wa NASA washiriki maandamano kwa wiki ya pili

0
2022
Polisi wakijitayarisha kuwakabili waandamanaji PICHA:MAKTABA COURTESY

Nairobi,KENYA: Wafuasi wa NASA wameanza maandamano ya kuwataka maafisa kadhaa wa tume ya uchaguzi IEBC wang’atuke uongozikwa kuhujumu uchaguzi wa mwezi wa nane.

Maandamano yameshuhudiwa mji wa Kisumu.

Huko Nairobi,maafisa wa polisi wanashika doria nje ya makao makuu ya IEBC huku waandamanaji wakianza kukusanyika.

Hapa Mombasa maandamano hayo yanatarajiwa kuongozwa na gavana Ali Hassan Joho.

Kinara wa NASA Raila Odinga alitangaza kuwa maandamano hayo yatakuwa yakifanyika kila jumatatu na ijumaa hadi maafisa hao wakiongozwa na mkurgenzi mkuu wa IEBC-Ezra Chiloba aondoke.

Comments

comments