Mbunge Babu Owino akamatwa tena

0
1971

Nairobi,KENYA:Mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino amekamatwa tena na polisi dakika chache baada ya mahakama ya Nairobi kumwachilia kwa dhamana.

Owino amekamatwa na polisi nje ya mahakama hiyo.

Lakini haijafahamika sababu za kukamatwa kwake.

Anakabiliwa na kesi ya kumtusi rais Kenyatta.

Awali aliachiliwa na kuagizwa kulipa bondi ya shilingi nusu milioni pesa taslimu.

Polisi walilazimika kuwafyatua gesi za kutoa machozi wafuasi wa mbunge huyo waliokuwa nje ya mahakama wakati mbunge huyo akikamatwa.

Comments

comments