IEBC yahakikishia wakazi Lamu uchaguzi utafanyika eneo hilo

0
1143

Lamu,KENYA:Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imewahakikishia wakazi katika maeneo yanayokumbwa na changamoto za kiusalama kaunti ya Lamu kwamba watashiriki kikamilifu Uchaguzi Mkuu  Agosti 8.

Afisa Msimamizi wa IEBC katika Kaunti ya Lamu, Mohamed Adan, anasema matayarisho kabambe yanaendelea ili kuona kila mkazi Lamu anapiga kura.

Anasema ofisi yake imefanya majadiliano na idara ya usalama ya kaunti ya Lamu na maafisa wa IEBC watakaosimamia uchaguzi hasa eneo la Basuba watakuwa wakisafirishwa kwa ndege hadi katika vituo vya kupiga kura.

Anasema juma hili watakuwa wakielekea Basuba na Pandanguo ili kutathmini hali maeneo hayo na pia kukutana na wakazi

 

 

Comments

comments