Rais Kenyatta bado ni maarufu kwa mujibu wa kura ya maoni

0
2023

Nairobi,KENYA:Utafiti wa hivi punde unaonyesha kuwa rais Uhuru Kenyatta bado anaongoza kwa umaarufu lakini mwanya kati yake na mpinzani wake Raila Odinga umepungua.

Utafiti huo wa kampuni ya Info Trak unaonyesha kuwa rais Kenyatta ana umaarufu wa asilimia 48 huku kinara wa NASA Raila Odinga akiwa na asilimia 43.

Abuda Dida ni wa tatu na asiilimia 0.5, Ekuru Aukot, Cyrus Jirongo na Joe Nyagah wanafuata kwa asilimia 0.1 kila mmoja.

Infotrak inasema utafiti huo ulishirikisha watu elfu mbili nchini katika maeneo bunge 29 kati ya tarehe 24-25 mwezi huu wa juni.

Utafiti huo unaonyesha kuwa rais Kenyatta ana umaarufu mkubwa maeneo ya kaskazini mashariki, mashariki, eneo la kati na bonde la ufa.

Raila ana ufuasi mkubwa pwani, Nyanza, Nairobi na magharibi.

Wakati huo huo nusu ya wakenya wanaamini kuwa nchi inaendeshwa vibaya,kwa mujibu wa utafiti huo.

Comments

comments