NASA kurudisha wadhifa wa waziri mkuu serikalini

0
1317
PICHA:HISANI

Nairobi,KENYA: Muungano wa NASA umezindua rasmi manifesto yake.

Katika manifesto hiyo, NASA itabuni nafasi ya waziri mkuu ambaye atakuwa na jukumu la kuunda baraza la mawaziri 20.

Wakati huo huo serikali hiyo pia itakuwa na manaibu mawaziri wasiozidi 20.

NASA pia inasema itaongeza mgao kwa serikali za kaunti hadi asilimia 45 ili kuhakikisha maendeleo mashinani.

Muungano huo aidha umeapa kutatua masuala yote ya ardhi ndani ya siku 100 baada ya kuchukua uongozi.

Kulingana na manifesto ya NASA, mawaziri watachaguliwa pia miongoni mwa wabunge.

Aidha NASA inasema itajenga daraja katika kivukio cha Likoni hapa Mombasa.

Comments

comments