Mwanahabari wa Baraka FM azoa tuzo za uandishi wa kawi

0
1724
Hillary Makokha (wa tatu kutoka kushoto) na wanahabari wengine wakipokea tuzo zao. PICHA:HISANI

Niarobi,KENYA: Mwanahabari wa Baraka FM ameshinda tuzo za uandishi bora.

Hillary Makokha alizoa tuzo mbili jumanne jioni katika mashindano ya uandishi bora wa masuala ya kawi na mazigira yaliyofanyika mjini Nairobi.

Mashindano hayo yalihudhuriwa na waziri wa kawi Charles Keter.

Makokha alishinda kutokana na makala yake iliyoangazia manufaa ya jikokoa.

Mshindi wa kila kitengo alipokea kikombe na hundi ya zaidi ya shilingi laki moja unusu.

Stesheni ya Baraka FM imesifika sana katika uandishi bora katika nyanja mbalimbali kutokana na ukakamavu wa wanahabari wake.

Kila mwaka, wafanyakazi wa kituo hicho hushinda katika mashindano tofauti ya uandishi bora.

Comments

comments