Raila akabidhi IEBC stakabadhi zake za kuwania urais

0
1058

Nairobi,KENYA:Kinara wa NASA Raila Odinga amekabidhi stakabadhi zake za uteuzi kuwania urais kwa Tume ya uchaguzi na mipaka IEBC mjini Nairobi.

Raila ameandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka pamoja na viongozi wa NASA wakiwemo gavana wa Bomet Issac Ruto, seneta wa Bungoma Moses Wetangula na kinara wa Amani-Musalia Mudavadi.

Hayo yakijiri IEBC imekataa kupokea stakabadhi za mgombea urais Abduba Dida.

IEBC inasema mgombea huyo amekosa kuwasilisha vyeti vya masomo ambavyo vimeidhinishwa na chuo alichosomea.

Wagombea wanane wa urais wameanza kuwasilisha stakabadhi zao leo kwa IEBC kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.

Rais Kenyatta atakabidhi zake hapo kesho.

Comments

comments