Msongamano wa magari Kibarani wakera abiria

0
2120

Mombasa,KENYA: Wasafiri wanaotumia barabara ya Kibarani hapa Mombasa wanaendelea kulalama kuhusu msongamano  wa magari.

Msongamano huo mkubwa unadaiwa kusababishwa na barabara mbovu eneo la Jomvu kuelekea Miritini.

Abiria wanalalamika kuwa safari ya dakika kumi na tano inawachukua zaidi ya saa mbili.

Sasa wanawataka wahusika kutafuta suluhisho la msongamano huo wakilalama kuwa wanapoteza muda mwingi barabarani kando na kugharamika zaidi kifedha.

Lakini afueni inatarajiwa pindi reli mpya ya SGR itakapoanza kubeba shehena za mizigo kutoka bandarini.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulizindua rasmi reli hiyo wiki ijayo.

Comments

comments