Watu 6 wafariki baada ya ukuta kuporomoka Mombasa

0
1398

Mombasa,KENYA: Watu sita wamefariki baada ya kuangukiwa na ukuta eneo la Pandya hapa Mombasa.

Watu hao ni mama na watoto wake wanne pamoja na mwanamme mmoja aliyekua akifanya kazi ya kuchoma mahindi eneo hilo.

Polisi wanasema huenda mvua kubwa inayoendelea kunyesha imesababisha mkasa huo.

Wakati huo daraja la Mbogolo barabara kuu ya kilifi-Malindi imefunikwa na maji kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Barabara hiyo haiwezi kupitika na hivyo wenye magari wanashauriwa kutumia njia ya Mavueni-Kaloleni ili kufika Mombasa

Comments

comments