Mombasa,KENYA: Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho jumatano anatarajiwa kaundiksiha taarifa na kitengo cha upelelezi CID kuhusu madai ya kughushi vyeti vya masomo yake.
Aidha gavana Joho ameikosoa serikali yan jubilee akisema inamwandama kila uchao.
Kulingana na Joho, idara hiyo ya upelelezi ilimwandikia barua ikimtaka afike ajieleze kuhusu madai hayo ya kughushi cheti chake cha kidato nchini.
Gavana Joho anasema masaibu yake yalianza pindi alipoanza kupinga mpango wa kuhamisha oparesheni za bandari ya Mombasa hadi Naivasha.
Akihutubia wanahabari hapa Mombasa, Joho alisema wanaomwandama sasa wameelekea hadi kiwango cha kuchunguza cheti chake cha kuzaliwa.
Kwingineko mbunge wa Nyali Hezron Awiti ametangaza kuhama chama cha wiper.
Mbunge huyo anadai huebnda uteuzi wa wagombea wa wagombnea wa gavana wa mombasa ukakumbwa na udanganyifu.
sasa anatarajiwa kuwasilisgha barua yake ya kujiuzulu na kutangaza wazi chama atakajiojiunga nacho.
Awiti ni miongoni mwa wagombea wa kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa kwenye uchaguzi mkuu ujao wa agosti.