Rais Kenyatta asema yeye na Raila sio maadui

0
1483

Nairobi,KENYA:Rais Uhuru Kenyatta ametetea serikali yake akisema imetekeleza miradi mingi ya maendeleo tangu aliochukua hatamu za uongozi mwaka 2013.

Akihojiwa na runinga moja nchini, rais Kenyatta amekiri kuwa wadhifa huo wa urais una changamoto nyingi lakini hajutii kuongoza nchi.

Kiongozi wa nchi pia amesema kuwa hana chuki na mwanasiasa yeyote akikariri kuwa tofauti zake na kinara wa upinzani Raila Odinga ni za kisiasa tu.

“Simchuki mtu yeyote.Mimi humwita ndugu yangu kila tukikutana.Tofauti za kisiasa sio uadui’, alisema rais.

Kuhusu ziara za nje ya nchi ambapo alishtumiwa na upinzani, rais Kenyatta alisema ziara hizo zilikua na manufaa kwa nchi.

Alitaja mradi wa kuwapa wakenya wa mapato ya chini stima na ujenzi wa barabara pamoja na upanuzi wa bandari ya Mombasa kama baadhi ya miradi ambayo yamebadilisha maisha ya wakenya.

Kuhusu ufisadi, rais Kenyatta alisisitiza kuwa alitekeleza wajibu wake kwa mujibu wa katiba.

Comments

comments