Mombasa, KENYA: Kenya jumatatu hii imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha wiki ya maombi hasa kwa waumini ya dini ya kikristo.
Huko mjini Mombasa viongozi wa madhehebu mbalimbali walitumia fursa hiyo, kuhimiza wakenya kuwa waangalifu na baadhi ya viongozi wa kiasasa wanaotaka kuwachochea, wakati huu taifa linapojianda kushiriki uchaguzi mkuu.
Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo la Mombasa Martin Kivuva, alitoa wito kwa wanasiasa kuhakikisha wanaendesha kampeini zao kwa njia ya amani.
Maombi hayo yanatarajiwa kukamilika jumamosi hii katika uwanja wa Tononoka mjini Mombasa.
Imeharirirwa na Joseph Jira