Mwanamme anayedaiwa kumuua mkewe akamatwa

0
1067

Mombasa,KENYA: Polisi eneo la Likoni mjini Mombasa inasema imemkamata mwanamume anayedaiwa kumuua mkewe mwaka jana.

Mshukiwa alitambulika kwa jina Mutua Mwanzia na anadaiwa kumuua mkewe Mary Wanjiku na kisha kuficha maiti yake chini ya kitanda.

Polisi walisema ofisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma imekamilisha uchunguzi na sasa inapendekeza mshukiwa ashtakiwe kwa kosa la mauaji.

Mkuu wa polisi wilayani Likoni huko Mombasa Willy Simba alisema mshukiwa atafunguliwa mashtaka ya mauaji.

Imeharirirwa na Joseph Jira

Comments

comments