Mvurya asalimu amri na kuondoa ada kwa wenye baa

0
903

Serikali ya kaunti ya Kwale imeahidi kufanya kikao na wamiliki wa baa na sehemu za burudani wanaopinga nyongeza ya ada za leseni za biashara zao.

Akizungumza na waandishi wa habari, naibu gavana wa Kwale Fatuma Achani amesema wanashughulikia swala hilo ili kuona kuwa nyongeza hiyo inaondolewa.

Mwenyekiti wa wamiliki baa kaunti hiyo Richard Onsongo anadai bunge la kaunti hiyo lina njama ya kusamabratisha biashara zao kutokana na hatua ya bunge hilo kuidhinisha ada hizo.

Wamiliki wa baa na vilabu wanataka ada hizo zifutiliwe mbali kutokana na janga la corona.

Comments

comments