Madaktari wa Mombasa wahepa wakihofia coronavirus

0
1193

Kizazaa kilizuka katika hospitali moja hapa Mombasa baada ya madaktari na wauguzi kutimka mbio baada ya wachina wawili kufika hospitalini humo kutaka kupimwa iwapo wana corona virus.

Kwa mujibu wa mhudumu mmoja ambaye hakutaka kutajwa, pindi wachina hao walipowasili wakiwa wamefunika midomo yao kwa kitambaa maalum na kutaka kupimwa, manesi na madaktari walianza kutimka mbio.

Mhudumu huyo anasema ilimchukua mhudumu mmoja mwenye ujasiri kuwaeleza wachina hao kwamba hawana vifaa vya kupimwa corona ambapo wachina hao waliondoka.

Baadae utulivu ulirejea hospitalini humo.

Comments

comments