Hoteli ya kifahari ya Leopard beach,Ukunda yachomeka

0
1424

Mali ya thamani isiyojulikana imeteketea baada ya moto kuzuka usiku wa kuamkia jumatatu katika hoteli ya kifahari ya leopard beach huko Diani  kaunti ya kwale .

Moto huo ulizuka mwendo wa saa tatu unusu usiku katika jengo moja la hoteli hiyo kisha  kusambaa kwa kasi katika majengo mengine matano ya hoteli hiyo.

OCPD wa Msambweni Joseph Chebusit amesema hakuna aliyejeruhiwa katika mkasa huo kwani wageni waliokolewa na kupelekwa katika hotel jirani  na  juhudi za kuuzima moto huo zilifaulu mapema.

Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo  kwani hasara ya mamilioni ya pesa inakadiriwa.

Comments

comments