Polisi wafumaniwa wakisafirisha pombe haramu

0
1257

Maafisa wawili wa polisi waliofumaniwa wakisafirisha pombe haramu wakitumia gari la polisi kutoka mpaka wa Kenya na Uganda eneo la Busia watashtakiwa mahakamani leo.

Maafisa hao wa AP walikuwa wakitumia gari la polisi kusafirisha pombe hiyo ya thamanani ya shilingi laki mbili pamoja na mwenye pombe hiyo.

Kamanda wa polisi eneo la Mumias Peter kattam amesema polisi hao walikamatwa katika kizuizi cha barabara baada ya raia kupiga ripoti.

Comments

comments