Meja mstaafu Twalib Mbarak amesema atashirikiana na asasi zate za serikali katika kukabili ufisadi ambao ni donda ndugu humu nchini iwapo atateuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa tume ya kukabili ufisadi EACC.
Akiongea alipohojiwa na kamati ya bunge, Mbarak pia ameahidi kuwaandama wafisadi hasa wa mali ya umma na kurudisha mali hiyo kwa wakenya.
Amesema iwapo ataidhinishwa kuchukua usukani katika EACC, chuma cha wafisadi ki motoni na wataandamamwa bila uoga wala huruma.
Mbaraka ambaye ni mzaliwa wa Kilifi, pia ameweka bayana autajiri ake akisema ni takriba shilingi milioni 152.
Amesema alipata mali hiyo kwa kuchukua mikopo wakati akiwa mwanajeshi na kuwekeza ndiposa utajiri wake ukakuwa.
Mbarak aliibuka bora katika mchujo wa kumtafuta mkurugenzi mpya kuchukua nafasi ya Halakhe Waqo.