Bodi kuchunguza unyanyasi katika reli ya SGR

0
1054

Bodi ya shirika la reli nchini imeanza kuchunguza madai ya ubaguzi wa rangi katika oparesheni za reli ya kisasa maarufu -SGR.

Hii ni kufuatia taarifa ya ufichuzi katika gazeti moja la humu nchini kwamba  wachina wanaosimamia SGR, wanabagua wakenya kwa misingi ya rangi pamoja na kuwadhulumu haki zao.

Katika ufichuzi huo, madereva wa Kenya bado hawajapewa nafasi ya kuendesha gari moshi hilo huku nafasi zote zikichukuliwa na wachina.

Hayo yakijiri mkurugenzi wa shirika la reli nchini–Atanas Maina ametetea gharama ya shilingi bilioni moja ya kuendesha SGR kila mwezi.

Comments

comments