Wakenya watatu waingia Somalia kujiunga na Al-shabaab

0
1111

Mombasa,KENYA: Idara ya usalama nchini inasema wakenya watatu wametorokea nchini jirani ya Somali na kujiunga na kundi la kigaidi la al shabaab.

Msemaji wa idara hiyo  Charles Owino ametaja majina ya watatu hao kama Mohamed Abdalla Asman, Hamis Hemed na Ali Ahmed Ali.

Amesema vijana hao wanatokea maeneo ya Malindi na Majengo-Nairobi  .

Owino  watatu hao walitoroka mapema jumatano wakisaidiwa na mmoja wa washukiwa wa ugaidi waliokuwa wakiwasiliana naye.

Amedokeza kuwa washukiwa hao huenda wakarejea nchini kupanga mashambulizi ya kigaidi.

Comments

comments