Hasara ya moto mkubwa Voi

0
1291

Voi,KENYA: Wafanyibiashara mjini Voi kaunti ya Taita Taveta wanakadiria hasara ya mamilioni ya pesa baada ya moto mkubwa kuteketeza eneo moja la biashara mapema hii jumatano.

Kwa mujibu wa naibu kamishena wa Voi Joseph Mtile,moto huo ulianza saa kumi na mbili unakisiwa kusababishwa na hitilafu za umeme.

Anasema chanzo cha moto huo kilitokana na kupotea kwa umeme kote nchini jana.

Wafanyibiashara hao wameitaka serikali ya kaunti na kampuni ya umeme nchini kuwafidia kutokana na hasara hiyo.

Pia  wamelalamikia hatua ya serikali ya kaunti hiyo kukosa mipangilio imara ya kukabiliana na majanga.

Comments

comments