Watoto wa miaka 7 na 13 wakamatwa kwa madai ya ujambazi

0
1179

Tana River,KENYA: Watoto watatu wa umri wa miaka 7 na 13 wamekamatwa mjini Hola kwa tuhuma za wizi.

Watato hao wamekamatwa baada ya taarifa kwamba walikuwa wamevunja duka la vifaa vya kielektroniki kabla ya mkazi kuarifu polisi.

Watoto hao wanashukiwa kuwa miongoni mwa watoto waliojiunga na kundi la watu wazima kutekeleza wizi.

OCPD wa eneo hilo Sylvester Githungo amesema watoto hao wamekuwa wakivunja maduka mjini Hola na kusababishia wafanyabiashara hasara kubwa.

Comments

comments