Gavana wa Nyeri Wahome Gakuru afariki

0
2503
Gavana wa Nyeri Wahome Gakuru. PICHA:HISANI.

Nyeri,KENYA: Gavana wa Nyeri Dr.Wahome Gakuru ameaga dunia.

Dr. Gakuru alifariki baada ya kufikishwa hospitali ya Thika Level 5 kufuatia ajali mbaya ya barabani mapema jumanne asubuhi eneo la Kabati, barabara ya Thika – Murang’a ambapo alijeruhiwa vibaya.

Dereva na Mlinzi wake pia walijeruhiwa katika ajali hiyo.

Gavana huyo alikua akielekea Mjini Nairobi kwa mahojiano katika kituo cha habari kabla ya ajali hiyo kutokea.

Naibu rais William Ruto ametoa risala za rambirambi kwa familia ya gavana huyo wa Nyeri.

Akizungumza alipofika katika chumba cha Lee ambako mwili wa gavana huyo umelazwa, Ruto amemtaja marehemu kama mtu aliyejitolea kutumia wakazi wa Nyeri na taifa kwa ujumla.

Comments

comments