Nairobi,KENYA: Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Wafula Chebukati amesema kuwa hawaezi kubadilisha kampuni iliyopewa zabuni ya kuchapisha makaratasi ya kupigia kura kufuatia malalamishi ya upinzani.
Chebukati anasema hilo haliwezekani kutokana na sababu za muda.
Anasema uchaguzi mkuu unakaribia kuandaliwa hivyo ni vigumu kuanza mchakato mpya wa kupeana zabuni kwa kampuni nyingine.
Chebukati amesema hayo kwenye mkutano na maagenti wa wawaniaji urais.
Muungano wa NASA unadai kuwa kampuni hiyo ya Dubai Al Ghurair iliyopewa zabuni hiyo ina uhusiano na Muhoho ambaye ni nduguye rais Uhuru Kenyatta.