Wagonjwa wataabika kufuatia mgomo wa wauguzi

0
1169
Hospitali ya Malindi.

Mombasa,KENYA:Madhara ya mgomo wa wauguzi uiliongia siku ya tatu leo yanaendelea kushuhudiwa.

Duru zinasema kuwa katika hospitali ya portreitz hapa Mombasa, wauguzi wamewaondoa kwa lazima wagonjwa 30 wa akili.

Inasemekana wameaachiliwa waende makwao.

Hapo jana wagonjwa 6 waliripotiwa kufariki katika hospitali ya Makadara.

Idadi ndogo ya wagonjwa imeshuhudiwa baada ya wauguzi hao kusitisha huduma zao.

Katibu mkuu wa wauguzi kaunti ya Mombasa Peter Maroko anasema wataendelea na mgomo wao hadi serikali itekeleze matakwa yao.

Huko Kilifi, wagonjwa watatu waliripotiwa kuangamia kwa kukosa matibabu.

 

Comments

comments