Seneta Ongoro agura ODM akidai kuonewa

0
1607
Mbunge wa Ruaraka bw Kajwang' na seneta Elizabeth Ongoro. PICHA:MAKTABA

Nairobi,KENYA:Katibu mkuu wa chama cha ODM Elizabeth Ongoro amekihama chama hicho.

Seneta huyo mteule ametangaza kugura ODM akisema amenyimwa nafasi ya kuwania wadhifa katika uchaguzi mkuu ujao.

Ongoro alizuiwa kugombea ubunge wa Ruaraka kama hatua ya kinidhamu baada ya wafuasi wake kupigana na wa mbunge wa eneo hilo TJ Kajwang katika mtaa wa Mathare mwezi jana. Watu wawili waliuawa katika mapigano hayo.

Hatua yake inakuja siku moja baada ya uongozi wa chama hicho kuwapa magavana 20 na viongozi wengine wapatao 850 tiketi ya moja kwa moja kuwania viti mbalimbali katika uchaguzi huo.

Bi. Ongoro anakuwa katibu mkuu wa pili wa chama ODM kuhama chama hicho.

Ababu Namwamba aligura ODM na kujiunga na chama cha Labour.

Comments

comments