Nairobi,KENYA:Viongozi wa kidini kutoka eneo la Nyanza wamejitokeza kumtetea kinara wa upinzani Raila Odinga dhidi ya matamshi ya rais Uhuru Kenyatta kuwa alihusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya wakenya 1300 waliuawa.
Askofu Mwai Abiero wa kanisa la kianglikana na Washington Ogonyo pia wanamtaka rais kukoma kutonesha kidonda ambacho wanasema kimeanza kupona.
Wakati huo huo wabunge John Mbadi, Timothy Bosire, Opiyo Wandayi, na mwakilishi wa wanawake kaunti ya Homa Bay Gladys Wanga wanamshtumu rais kwa kuzua uchochezi dhidi ya Raila.
Rais alinukuliwa katika ziara yake kaunti ya Kisii akisema kuwa Raila alihusika na ghasia hizo.
Hata hivyo, Raila alimjibu rais akisema anajaribu kujitetea kwa umma baada ya kushindwa kutekeleza ahadi za jubilee kwa wananchi.
Raila pia alimweleza rais kuwa watu wanaomzingira ndio waliohusika na ghasia hizo.