Washukiwa zaidi waliovamia kituo cha polisi Kwale wakamatwa

0
1424

Kwale:KENYA: Polisi inasema imewakata washukiwa wengine wawili zaidi wa shambulizi la kituo cha polisi cha Kombani kaunti ya Kwale.

Idadi hii iliongezeka na kufikisha washukiwa 3 waliokamatwa kufikia sasa.

Taarifa zilisema washukiwa hao wawili walikamatwa siku ya alhamisi karibu na eneo la Kombani na maafisa wa kupambana na ugaidi.

Washukiwa hao wanatarajiwa kuhojiwa katika makao makuu ya polisi mjini Mombasa.

Mnamo siku ya jumamosi desemba 24 washukiwa wanaokisiwa kuwa 10 na ambao walikuwa wamejihami kwa panga na visu walishambulia polisi na kuwajeruhi maafisa watatu.

Mmoja wao alipigwa risasi na kufariki papo hapo.

Imehaririwa na Joseph Jira

Comments

comments